Tutatoa ushirikiano kuipa thamani Mwanamke Awards Tanga

Serikali Mkoani Tanga imeahidi kutoa Ushirikiano kwa Waandaji wa Mwanamke Awards mkoani humo ili kuongeza ufanisi na ubora zaidi kwa miaka ijayo ili kuweza kuwafikia Wanawake wengi zaidi ambao ni Wajasiriamali wanaofanya vizuri katika Sekta mbalimbali za Maendeleo.

Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya amewapongeza waandaaji wa Mwanamke Awards kwa kuweza kuongeza idadi ya Vipengele vinavyowania tuzo hizo kutoka Vipengele nane mwaka 2023 hadi kufika 15 mwaka 2024

Kwa Upande wake Muandaaji wa Mwanamke Awards mkoa wa Tanga Ashura Shamte amesema Miongoni mwa vipengele ambavyo washiriki walikuwa wakiwania ni pamoja na Huduma za Jamii, Mfanyabiashara Chipukuzi, Wajasiriamali Chipukuzi, Mfanyabiashara wa Mwaka, Mjasiriamali wa mwaka, Mpambaji bora wa Mwaka, Make Up Artist, Kazi za Mikono, Spices, Mwanamitindo wa Mwaka, MC wa Mwaka, Mhamasishaji wa Mwaka, na Malkia Awards

Aidha ameiomba Serikali Kuhamasisha viongozi wa Wilaya kuwaibua wanawake wengi zaidi ili waweze kushiriki katika Tuzo za Mwaka 2025

Kwa upande wake Mshindi wa Tuzo ya Mwanamitindo bora wa Mwaka Victoria Martin amewashukuru waandaaji na washiriki kwenye Vipengele vya Mwanamke Awards 2024 kwa kuendelea kushirikiana ambapo itasaidia kuutangaza mkoa wa Tanga kitaifa na Kimataifa

Related Posts