Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

RAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo kuandaa katazo la kupiga marufuku kwa taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100 kutotumia kuni na mkaa kuanzia Agosti mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endele).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumatano jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi kwa kupikia.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Katika miezi mitatu ijayo, Waziri mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Seleman Jafo, ofisi yako iandae na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kuhusu majaribio ya taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100 kuacha kutumia kuni na mkaa.

“Wamejaribu wameweza. Wale waliobaki hawataingia kama hakuna katazo, sasa uandae katazo kwa taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100 kwamba ni marufuku kutumia kuni na mkaa,” amesema Rais Samia.

Related Posts