Fadlu hana wasiwasi kuwavaa Bravos

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids, amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Bravos do Maquis na ataingia na mfumo wa kushambulia zaidi ili kupata ushindi.

Mchezo huo wa kwa kwanza wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika, unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ambapo kocha huyo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Fadlu ameeleza kuwa wanajua wanakwenda kucheza na mpinzani mgumu lakini kama benchi la ufundi pamoja na wachezaji wamejipanga kuonyesha mchezo mzuri ili kuanza vema hatua hiyo.

Kwa upande wake mchezaji wa kikosi hicho, Che Malone amesema wataingia uwanjani kutimiza kile walichoelekezwa na benchi la ufundi.

Related Posts