MASTAA KIBAO ALBAMU MPYA YA ERIC BELLINGER

NA JOSEPH SHALUWA

ALBAMU mpya ya staa wa muziki nchini Nigeria, Eric Bellinger inayokwenda kwa jina la ‘It’ll All Make Sense Later’ imewashirikisha mastaa kibao akiwemo Burna Boy ambaye ana Tuzo ya Muziki ya Grammy.

Mastaa wengine walioshirikishwa kwenye albamu hiyo ni pamoja na mkali wa RnB kutoka Ghana, Gyakie na mastaa wengine kutoka Nigeria ambao wamepata kushinda Tuzo ya Grammy – Reekado Banks, Oxlade, Tempoe na Taves.

Usisahau kwamba, Eric Bellinger naye pia amepata kushinda Tuzo ya Grammy. Albamu yake hiyo inapatikana katika mifumo mbalimbali ya kidigitali mitandaoni.

Albamu yake hiyo iliyotengenezwa jijini Cape Town, Afrika Kusini, ndani yake ina mikong’osia ya aina yake yenye ladha za Kiafrika katika mitindo ya R&B, Afrobeats, na Amapiano.

Akizungumzia albamu hiyo, Eric anasema: “Nilisafiri hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kutengeneza hii albamu. Hii ni moja ya kazi iliyonipa uzoefu mkubwa sana katika utengenezaji wa muziki.

“Ni kazi nzuri hakika. Inanipa nguvu ya kusonga mbele, kujiamini katika kazi zijazo, ndiyo maana nimeiita hii albamu, ‘Italeta Maana Baadaye – It’ll All Make Sense Later.”

Akaongeza: “Naamini hii albamu itakonga nyoyo za mashabiki wangu.”

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo na wasanii walioshirikishwa kwenye mabano ni Pure, Special (feat. Konshens), Feelings Never Die na
Shooting Star (feat. Oxlade).

Nyingine ni Precision (feat. Reekado Banks), Backtrack (feat. Taves), Don’t Shut Off The Lights na For The Evening (feat. Burna Boy).

Vibao vingine ni Ms Africa (feat. Gyakie), Desire, Follow Her Lead, No Coincidence (feat. Geko), Top Dolla (feat. Vscript), Don’t Leave  na Unfinished Business. 

Wanamuziki wengine aliowahi kupiga nao kolabo ni Usher Raymond, Justin Bieber, Ne-Yo, bila kuwasahau Chris Brown na OG Parker.

Aidha, Eric amepata kuandika mashairi ya nyimbo na kuwatayarishia wasanii kama Chris Brown (“Indigo”, “New Flame”, “Champion”), Teyana Taylor (“69”, “How You Want It” feat. King Combs) na Usher Raymond (“Lemme See” feat. Rick Ross).

MJUE ZAIDI ERIC BELLINGER 

Eric Bellinger ni mwanamuziki mwenye Tuzo ya Grammy – Mwanamuziki Bora, Mtunzi Bora na Mtayarishaji Bora.

Anajulikana zaidi kwa nyimbo zake kali zilizotamba kama “Valet” aliopiga kolabo na Fetty Wap & 2 Chainz, “G.O.A.T” aliomshirikisha Wale na “Type a Way” aliofanya na Chris Brown na OG Parker. Eric amekwishatoa nyimbo zaidi ya 300 ndani ya albamu zake 40 alizoachilia hadi sasa.

https://ericbellinger.lnk.to/IAMSL

Related Posts