Dar es Salaam. Mbunge wa Kigamboni (CCM), DK Faustine Ndugulile amefariki dunia leo Jumatano, Novemba 27, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson. Amesema taarifa zaidi kuhusu msiba huo itatolewa.
Dk Ndugulile alikuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Dunia Kanda ya Afrika (WHO) ambaye alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
Endelea kufuatilia Mwananchi.