Ndege ya mizigo yatua kwa dharura mjini Istanbul baada ya gia kufeli kufanya kazi

Ndege ya mizigo ilitua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul siku ya Jumatano baada ya gear zake za mbele kushindwa kufanya kazi.

Video kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha ndege hiyo aina ya Boeing 767 mali ya FedEx Express ikitumia gia ya kutua nyuma na kugonga sehemu yake  ya mbele ya fuselage.

Ndege hiyo ilikuwa katika hatua ya mwisho ya safari yake kutoka Paris hadi Istanbul wakati marubani walipogundua kuwa vifaa vya kutua vya mbele vilishindwa kufunguka, Shirika la serikali la Anadolu lilisema.

Hakuna aliyejeruhiwa na wafanyakazi waliiondoa ndege hiyo wakiwa salama, amesema Abdulkadir Uraloglu, waziri wa uchukuzi na miundo mbinu wa Uturuki.

Njia ya kurukia ndege ilipotua ilifungwa wakati ndege hiyo ikiondolewa, alisema

Related Posts