Timu ya taifa ya kriketi yajifua bondeni

Baada ya mazoezi ya kina kwa kutumia timu za Ruaha na Tarangire, wachezaji wa timu ya taifa ya wanwake ya kriketl imeanza mafunzo zaidi ya kiufundi nchini Afrika ya Kusini.

Kwa mujibu wa msemaji wa Chama cha Kriketi nchini (TCA), Ateef Salim, timu hii imepiga kambi katika mji wa Pretorial baada ya kuondoka nchini mwishoni mwa juma.

“ Timu iko nchini Afrika kwa mafunzo ya kina ya kitalaam yanayoitwa High-Performance Training Program. Wachezaji hufundishwa mbinu za kisasa za uchezaji kriketi,” alifafanua Salim.

Wachezaji waliochaguliwa baada ya kukamilika zoezi la mchujo;  ni Swaumu Godfrey, Fatuma Kibasu, Neema Justine, Nasra Hamza na Perice Zakayo

Wengine ni Tabu Saidi, Nasra Nassoro, Hudaa Mrisho, Gertrude Mushi na Shufaa Hamza.

Vilevile katika orodha wapo Linda Justine, Sophia Frank, Mwanamvua Hamisi na  Adolphija Jeremiah.

Kwa mujibu wa TCA, timu hii tayari imeanza mazoezi katika viwanja Irene Country Club, na zoezi  kuu ni mafunzo  ya kina na uendelezaji vipaji.

“Hii ni hatua muhimu sana kwa timu na wachezaji wetu,  na sisi tunawataka wazingatie mafunzo ili tuwe na timu bora kwa michuano ya kimataifa,” alisema Salim.

Kabla ya kuondoka kwenda Afrika  Kusini wachezaji nyota wa kike wa kriketi walicheza mechi tano za mchujo wakijigawa kwa timu za Ruaha na Tarangire.

Katika michezo hiyo, Ruaha walishinda michezo minne na Tarangire kushinda mmoja.

Related Posts