Waziri Mkuu apiga kura kijijini kwake Nandagala

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 27, 2024 ameshiriki katika zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa, Lindi Novemba 27, 2024.

Akizungumza baada ya kupiga kura ambapo aliongozana na Mkewe Marry Majaliwa, Waziri Mkuu amewapongeza wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi kuchangua viongozi katika uchaguzi huo unaofanyika nchi nzima.

“Wananchi wamejitokeza kwa wingi, tayari mimi na familia yangu tumepata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye tunaamini atatuletea maendeleo kwenye kijiji chetu”.

Related Posts