Wasanii wa vichekesho watawala Kwa Mkapa

IKIWA imesalia saa Moja kabla ya kuanza kwa mchezo wa Kombe la shirikisho kati ya Simba dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola, wasanii mbalimbali wa vichekesho tayari wameshawasili uwanjani hapa.

Wasanii hao ambao baadhi wamevalia jezi za Simba ni pamoja na Asma Majeed, Mwaisa, Oka Martin na Carpoza.

Mbali ya hao pia yupo muigizaji wa Bongo Movie ambaye ni shabiki wa Simba Gabo Zigamba.

Hii inakuwa ni mechi ya ufunguzi kwa Kundi A ambalo mbali ya Simba na Bravo pia zipo CS Constantine na CS Sfaxien ambazo zitacheza saa 1:00 usiku.

Related Posts