Wananchi wa Mwanza jitokezeni kushiriki katika kutimiza haki ya kidemokrasia na kikatiba ya kupiga kura :RC Said Mtanda

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amewataka wananchi wa Mwanza kujitokeza kushiriki katika kutimiza haki ya kidemokrasia na kikatiba ya kupiga kura licha ya kuwepo na hali ya mvua na kuwataka hali hiyo isiwatie uvivu.

Mtanda amesema hiyo mapema leo Novemba 27, 2024 mara baada ya kushiriki zoezi la upigaji kura na kusisitiza umuhimu wa zoezi hilo kwa kuwa ndio daraja kati ya wananchi na Kiongozi kwa ngazi ya mwanzo kabisa.

Ameongeza kwa kusema kuikimbia mvua ya siku moja ni kukimbilia matatizo ya kuwa na kiongozi asiye thabiti kwa miaka mitano ni bora wajitokeze kupiga kura kwa muda mfupi kisha waendelee na shughuli zao.

Aidha Mkuu huyo wa Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika Mkoa wa Mwanza wamekubaliana kuwa Kiongozi atakayetangazwa ni yule atakaeshinda.

 

Related Posts