Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv
BAADHI ya wananchi wameonyesha kutokuwa na elimu ya kutosha ya upigaji kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaendelea nchini kiasi cha kuomba msaada kwa wapiga kura wenzao na wasimamizi.
Michuzi Tv mapema leo imeshuhudia baadhi ya wananchi wakihangaika kutafuta msaada wa kupiga kura katika vituo vya Tegeta Nyuki, Kopa Cabana, Wazo Hill na Bunju B hali iliyowapa wakati mgumu wa kutimiza haki yao ya kupiga kura.
Wananchi hao waliamua kuomba msaada huo kufuatia majina ya wagombea kuwa hafifu, kukosekana kwa majina yao na majina kuandikwa kwa kutofuata mpangilio wa herufi.
Akizunghmza na Michuzi Tv mkazi wa Wazo Hill, Mwanahawa Juma amesema ameshindwa kupiga kura kutokana na utaratibu mbaya wa utambuzi wa majina uliowekwa na wasimamizi lakini baada ya kuoata msaada akafanikiwa kupiga kura.
Naye Rashid Hussein mkazi wa Boko Magengeni jijini Dar es salaam amesema wameshangaa kuona karatasi ya kupigia kura ikiwa haina mgombea wa upinzani ili hali alikuwepo na kampeni kafanya hadi mwisho.
“Ni suala la kusikitisha sana kwani kwenye karatasi unakuta mgombea mmoja alafu kivuli wakati mtu alifanya kampeni mwanzo,mwisho hii inakatisha tamaa sababu kama mtu alimtaka huyo uliemtoa itakuwaje ni vyema awepo iliwananchi waamue yupi awaongoze,”amesema Hussein.
Pamoja na changamoto hizo wananchi kutoka maeneo mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kupiga kura katika maeneo yao ilikupata viongozi wa serikali za mitaa watakaowaongoza kipindi cha miaka mitano.
“Wananchi tumefika muda mrefu lakini majina hakuna,msimamizi anasema nendeni kituo kingine unafika napenyewe jina halipo sasa nifanye nini kingine zaidi ya kurudi nyumbani nikaendelee na majukumu mengine,”ameongezea Juma