Dar es Salaam. Aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni (CCM) na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Dk Faustine Ndugulile anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Desemba 2, 2024 Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Ratiba ya mazishi hayo imetolewa na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo imesema, Rais Samia Suluhu Hassan atawaongoza viongozi na wageni mbalimbali kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee kabla ya mazishi hayo.
Pia, ratiba hiyo imesema Dk Ndugulile ambaye alikuwa anatibiwa India, mwili wake utawasili nchini kesho Desemba 29, 2024 kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia
Dk Ndugulile alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Endelea kufuatilia tovuti ya Mwananchi