Ujio madaktari bingwa Morogoro mkombozi kwa wananchi

Baada ya timu ya madaktari bingwa 55 wa Dokta Samia Sukuhu Hasaan kuwasili mkoani Morogoro Kwa ajili ya kuanza kutoka matibabu ya kibingwa wakazi wa Mji huo wameshukuru huduma hiyo na kusema kuwa inasaidia Kwani huduma hizo wangezipata hospitali zingine Kwa gharama Kubwa.

Amina Juma ni mmoja wa wagonjwa waliofika katika.hospitali hiyo anasema akikua anasumbuliwa na magonjwa kwa zaidi ya miaka sita lakini alivyofika katika Kambi hiyo amepata huduma kwa Bei nafuu na sasa anaendelea na matibabu ambapo ameishukuru Serikali kwa utaratibu huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima amemwomba Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaongezea muda Madaktari Bingwa aliowaleta Mkoani Morogoro kutoa matibabu kwa wananchi (Outreach Services) ambapo wananchi wengi wameonekana wana uhitaji wa kuonana na Madaktari hao, hivyo amemwomba Dkt. Samia kuwaongezea muda ili kukidhi kiu
ya wananchi wake.

Mhe. Malima ametoa ombi hilo Mei 7, Mwaka huu wakati akizindua rasmi Kambi ya huduma za matibabu za Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Kanda ya kati zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuanzia Mei 6 na 10, 2024.

Sambamba na hilo, Mhe. Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kuwawezesha madaktari Bingwa 55 kupitia Wizara ya Afya kushiriki katika kambi hiyo aliyoiita ni kambi kubwa kuliko kambi zote alizowahi kuziona kwa kipindi chote alichofanya kazi Serikalini.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Hospitali kutoka Wizara ya Afya Dkt. Caroline Damian Mayengo amesema Wizara ya Afya itaendelea kuratibu mazoezi kama hayo kwa sababu ya mwitikio wa wananchi ni mkubwa hali inayoonesha kuna uhitaji huo wa wananchi kupata matibabu.


Aidha, amebainisha kuwa hadi kufikia Mei 7, 2024 tayari idadi ya watu zaidi ya 7000 kwa nchi nzima wamefikiwa na zoezi hilo la kupata matibabu kupitia kambi mbali mbali hapa nchini zinazoendelea kutoa huduma kama hiyo kupitia Madaktari
Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba hadi kufikia siku ya ljumaa ya Mei 10, 2024 watu wengi watakuwa wanufaika wa kambi hizo.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Pwani (Tumbi) Dkt. Aman Kighoma Malima ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kambi ya Kanda ya Kati amesema, Kambi hiyo inayojumuisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida, pwani na Morogoro.

Related Posts