‘Yanga tunaweza kununua Samia Infrastructure Bond’- Rais wa Yanga Hersi

Ni November 29, 2024 ambapo Benki ya CRDB inazindua rasmi SAMIA INFRASTRUCTURE BOND katika Ukumbi wa Mikutano Mlimani City Hall jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa waliohudhuria ni David Kafulila, Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi – PPP.

“Malengo ya Serikali ni kujenga uchumi ambao ni jumuifu, kwenye kujenga uchumi jumuifu lazima uhakikishe kwamba watu wengi wanashiriki kwenye uwekezaji ambao unafanywa na serikali ama sekta binafsi. Utaratibu wa hatifungani kwa ajili ya miundombinu unatoa nafasi ya watu wengi zaidi kuwa wawekezaji kwenye miundombinu. Utartibu huu ni kwamba CRDB wanatengeneza, hii hatifungani inanunuliwa na watu, kwa maana hiyo mimi nakuwa muwekezaji, kwa shilingi laki tano na mimi nasema nimekuwa muwekezaji kwenye sekta ya ujenzi, hii inajenga uchumi jumuifu” – David Kafulila, Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi – PPP.

Related Posts