‘Tusipoteza nguvu kazi ya Taifa kwa nishati chafu’ Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan amesema nguvu kazi ya Taifa ambao ni Watanzania zaidi ya elfu 33 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua ambayo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na uvutaji wa moshi kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Rais Samia amesema hayo leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam wakati wa hafla ya Uzinduzi uzinduzi wa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024 – 2034.

Pia Rais Samia amesema kwa kuwa akina mama ndio waathirika wakubwa wa nishati chafu, mkakati wa matumizi ya nishati safi utasaidia kuokoa kundi hilo na magonjwa pamoja na kuwakomboa kiuchumi.

Aidha Rais Samia amesema takribani hekta 469,000 za misitu (karibu sawa na ukubwa wa Jiji la Dar es Salaam) hupotea kila mwaka, chanzo moja wapo ikiwa ni ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Rais amesema hali hiyo hufanya upatikanaji wa kuni na mkaa wakati mwingine kuwa wa shida kuliko kutafuta chakula.

Related Posts