Mahakama yamuachia huru aliyekuwa RC Simiyu

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahya Nawanda katika kesi ya kulawiti iliyokuwa inamkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Uamuzi wa kesi hiyo namba 1883/2024, umetolewa leo tarehe 29 Novemba 2024, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Erick Marley.

Akisoma uamuzi huo, hakimu alisema kuwa baada ya kupitia ushaidi na vielelezo vilivyowasilishwa kwenye shauri hilo, Mahakama imejiridhishwa kuwa, hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia mshtakiwa na kuamua kumuachia huru.

Dk. Nawanda alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, tarehe 09 Julai 2024, na kosemewa shtaka hilo na waendesha Mashtaka wa Serikali, Magreth Mwaseba na Martha Mtiti.

Kwa mujibu wa Mwaseba alieleza Mahakama hiyo kuwa, mshtakiwa alidaiwa Kutenda kosa hilo tarehe 02 Juni 2024, kwenye eneo la maegesho ya magari lililoko Rock City Mall wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Aliendelea kusema kuwa Kutenda kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 154 (1)(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.

Mara baada ya kuachiwa huru na Mahakama hiyo, Dk Nawanda aliwaambia waandishi wa Habari kuwa, Mahakama imetwenda Haki hivyo anamshukuru Mungu.

“Namshukuru Mungu, Familia Yangu na Mahakama imetenda Haki, Mungu ni Mwema kila kitu kinatoka kwa Mungu, utukufu ni wake Mungu.”alisema Dk. Nawanda.

About The Author

Related Posts