BODI MPYA UONGOZI INSTITUTE YAZINDULIWA, WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA MAELEKEZO

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

BODI Mpya ya Taasisi ya Uongozi Institute ambayo imezinduliwa rasmi leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Simbachawene imeshauriwa kuweka mikakati itakayofanikisha Taasisi hiyo inakuwa na sura ya Bara la Afrika.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 28,2024 alipokuwa akizindua bodi Mpya ya Uongozi Insitute ambayo imeteuliwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan , Waziri Simbachawene amesema kwa mujibu wa Sheria na maisha yake ni miaka mitatu, hivyo amewapongeza wajumbe wa tume hiyo kwa kuaminiwa na Rais.

“Taasisi ya Uongozi ni ya Bara la Afrika na kwa bahati tu kwamba Tanzania na nchi ya Finland ndizo nchi mpaka sasa hivi zinachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Taasisi hii na wengine wanaendelea kuingia katika program zinazotolewa za uongozi katika Taasisi hii ni nyingi na zinaanza kutanuka.

“Na malengo ambayo nimewapa ambayo pia Rais Samia ameelekeza ni kwamba Taasisi ipate sura ya bara la Afrika kwasababu msingi wa kuanzishwa kwake ilikuwa kujenga uwezo wa viongozi kwa bara la Afrika ili kuwa na mipango na malengo endelevu ya maendeleo katika Bara la Afrika kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuboresha maisha ya wana bara la Afrika .

“Nimezindua bodi hii na tunamshukuru Rais Dk.Samia kwa kututeulia bodi nzuri ambayo inamchanganyiko wa mataifa mbalimbali na tunaamini itakuja na kitu kipya ili kutekeleza malengo ya kuanzishwa kwake,”amesema.

Ameongeza miongoni mwa mambo ambayo bodi hiyo inatakiwa kutekeleza ni kuendelea na kazi ya msingi ambayo ni kujenga uwezo wa viongozi wa Afrika waliopo na wanaokuja na ndio maana mafunzo yanahusisha kujenga uwezo wa kiungozi kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi walioko madarakani.

Amesema ndio maana utawakuta katika shughuli za taasisi huwa kuna midahalo inafanyika kwa viongozi wakubwa wa nchi,marais hushiriki midahalo hiyo lakini pia kutolewa mafunzo kwa viongozi walioko katika ofisi mbalimbali ili kuwawezesha kutoa huduma ambazo zinakwenda na wakati na hilo ndio jambo kuu .

Kwa Upande wake Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo ambaye ameingia kipindi cha pili kuongoza bodi hiyo,Balozi Ombeni Sefue amesema kuzinduliwa kwa bodi hiyo pamoja na shughuli zake za msingi pia itaendeleza kazi nzuri zilizofanywa na bodi iliyopita.

Balozi Sefue amesema mpango mkakati uliopo sasa ni ule wa bodi iliyopita ambao umebakisha mwaka mmoja kumalizika na Kisha bodi itakuwa na kazi ya kuandaa mkakati utakaofata.

“Tunayo mikakati ikiwemo ya kuongeza programu mpya kuandaa wanawake katika uongozi,Programu ya kuboresha utendaji wa mashirika ya umma na programu maalum ya usimamizi wa mashirika ya umma ambayo ni programu mpya kwa kushirikiana na ofisi ya hazina.”

Pia amesema Uongozi Institute imekuwa ikiendelea na program za mafunzo kwa viongozi mbalimbali na kuongeza pamoja na programu hizo wamekuwa wako angalia nahitaji ya Dunia ili kuandaa viongozi wanaokwenda na wakati.” Lazıma tuandae viongozi kwa ajili ya leo na kesho na kwa mazingira hayo huwezi kuwa na viongozi ambao Mawazo yao yako jana badala ya kuwa na mawazo.”

 

Related Posts