Australia yapiga marufuku mitandao ya kijamii kwa watoto

Australia imepitisha sheria inayopiga marufuku watoto walio chini ya miaka 16 kutumia mitandao ya kijamii, hatua inayolenga kulazimisha kampuni za teknolojia kuboresha usalama.

Sheria hiyo, iliyopitishwa na seneti Alhamisi usiku Novemba 28, 2024, inazihitaji kampuni kama Snapchat, TikTok, na Instagram kuchukua kuhakikisha watoto hawapati huduma zao, vinginevyo zitalipishwa faini ya hadi Dola milioni 50 za Australia.

Waziri Mkuu, Anthony Albanese amesema, “Majukwaa haya sasa yana jukumu la kijamii kuhakikisha usalama wa watoto ni kipaumbele kwao.” Ameongeza kuwa mitandao ya kijamii inaweza kuwa silaha ya wanyanyasaji, chanzo cha msukumo wa rika, na zana ya wanyanyasaji wa mtandaoni.”

Muswada huo umeungwa mkono wa upinzani, huku Seneta Maria Kovacic akisema ni “Wakati muhimu kwa Taifa letu kuwalinda watoto.” Hata hivyo, Seneta Sarah Hanson-Young alieleza hofu yake kuwa mchakato ulikuwa wa haraka.

Licha ya ukosoaji huo, asilimia 77 ya Waustralia wanaunga mkono sheria hiyo, huku serikali ikitarajia kutangaza tarehe rasmi ya kuanza utekelezaji.

Je, unafikiri hii inapaswa kuja na hapa Tanzania tuandikie maoni yako?

Related Posts