WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Riadhaa ya Climate Change 2024 yatakayofanyika wilayani Pangani kesho Novemba 30 mwaka huu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Tree Of Hope kwa kushiriana na Asasi nyengine za Mtandao wameandaa mbio hiyo fupi katika Mji Mkongwe wa Pangani na wageni kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani watashiriki.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya alisema maandalizi ya mbio hizo yamekamilika na yamefikia zaidi ya asilimia 90 ambapo wanatarajia Waziri Dkt Ashatu Kijaji kuwasili wilayani humo akiwemo Rais wa Chama cha Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka,
Msuya alisema kwamba kwa upande wa njia ambazo zitatumika kwa wakimbiaji hao zipo katika hali nzuri na maeneo ya malazi yapo vizuri huku akisisitiza suala la ulinzi na usalama limeimarishwa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa.
Alitaja mbio ambazo zitakimbiwa na wakimbiaji kuwa ni zile zenye umbali wa Kilomita 21,Kilomita 10 na Kilomita 5 ambapo wakimbia wasiopungua 300 kutoka Tanzania Bara na Visiwani wanatarajiwa kushiriki mbio hizo.
Aidha aliwakaribisha wadau wote wa mbio na mazingira huku akieleza lengo lake ni kushirikisha wadau wa mazingira kuchangia upatikanjaji nishati safi ya kupikia ikiwa kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu ambaye ndie kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupika katika Taifa ,Africa na Duniani .
Hata hivyo alisema kwamba wanatarijia kupata majiko ya gesi na nishati mbadala kwa kaya mbalimbali hasa zile ambazo hazijiwezi kutumia nishati safi kwa sababu ya kipato.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Tree Of Hope Fortunata Manyeresa kwamba kupitia mbizo hizo wanakwenda kuleta hamasa mpya na kujenga uelewa wa jamii kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake
Manyeresa alisema pia itawajengea wananchi uhimilivu na ustahilimivu kwa masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi na wanaamini kwamba yana athari kubwa kwa jamii na yanawalenga sana wanawake.
Alisema kwa sababu mwanamke ndio wanakwenda kutafuta kuni na maji na usalama wa chakula nyumbani ukiwa dhaifuna kukiwa hakuna chakula watoto wanakwenda kumuambiwa mama.