Luhende asema tatizo mademu | Mwanaspoti

BEKI wa zamani wa Yanga na Mtibwa, David Luhende amesema changamoto inayowapoteza mastaa wengi wa soka kwa sasa ni starehe kupitiliza wanazofanya ikiwemo mademu.

Staa huyo ambaye anaitumikia Kagera katika msimu wa tano amekuwa panga pangua katika kikosi, huku akiwa na rekodi ya mabao saba.

Alisema mchezaji akiwa karibu na mitandao ya Kijamii, starehe za vilevi na zinaa kupita kiasi ni lazima aanze kushuka kwani hakuna kiwango bila jitihada na kuheshimu kazi.

“Vijana wa sasa watakaochezwa kwa muda mrefu kama sisi watahitaji pongezi, maana wakati wetu hatukuwa na vitu ambavyo vinaweza kuchukua muda mwingi kuliko mazoezi,” alisema.

“Vitu kama simu walikuwa navyo watu wachache sana, lakini kuwa na wanawake wengi ambao wanachangia kudhoofisha kipaji cha mchezaji. Kuna vitu vingi lakini starehe zimekuwa nyingi nje ya mpira na imekuwa ngumu kwao kuacha.

“Haimaanishi sisi ndio tunaishi sana ila ukiwaangalia waliodumu kwenye soka utagundua wanaishi maisha ya misingi ya soka., wengi wanaishia misimu mitano.”

Related Posts