Amza aibua jambo lao mazoezini

MSHAMBULIAJI wa Namungo FC, Moubarack Amza amesema kulingana na nafasi iliyopo timu wanahamasishana kupambana mazoezini ili kumpa urahisi kocha Juma Mgunda kupanga kikosi cha ushindi.

Namungo itaikaribisha Yanga kesho katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Namungo ipo nafasi ya 13, imecheza mechi 11 imeshinda tatu, imefungwa michezo minane na ina pointi tisa, kitu ambacho Amza anakiona wana kazi ya kuhakikisha wanapanda nafasi za juu.

Alisema anajitahimini ni namna gani kiwango chake kinavyoweza kuisaidia timu kufikia malengo na jinsi kocha anavyoonyesha kuwataka wapambane zaidi, ni vitu vinavyompa ari ya kujituma zaidi.

“Ni msimu mgumu unaohitaji kujituma kwa bidii, ndio maana kila mchezaji anakuwa anajitathimini kuhakikisha, kitu gani anapaswa kukifanya kwa ajili ya timu kuyafikia malengo yake,” alisema Amza ambaye msimu uliopita alimaliza na mabao matano.

Kuhusiana na msimu huu kwake bado anaona hajaunza kutokana na kutofunga katika mechi tano alizoanza na mbili aliingia kipindi cha pili akitoka kuuguza majeraha.

“Baada ya kurejea kutoka katika majeraha, nimeingia mechi mbili kipindi cha pili, naamini nitafunga katika michezo ambayo imesalia mbele yetu,” alisema.

Related Posts