Jospin Magambo ni katibu wa ofisi ya mamlaka ya serikali katika eneo la Minova wilayahi Kalehe. Anathibitisha kutokea kwa tukio hili na anakumbusha matukio mengine ya mashambulizi ya mabomu huko Minova, hali ambayo inaongeza wasiwasi kwa raia:
Soma pia: Hali ya usalama inazidi kuwa mbaya Goma
Msemaji wa jeshi la Kongo katika jimbo la Kivu Kusini, Luteni Dieudonné Kajibwami, alikataa kuithibitishia DW kutokea kwa mashambulizi hayo, lakini alisema anafuatilia tukio hili ili kutambuwa kwa kina yaliyojiri.
Tukio hili lilijiri muda mfupi baada ya wengine watu 18 kuuawa katika mashambulizi ya hivi majuzi katika kambi nne za watu waliokimbia makaazi yao mashariki mwa mji wa Goma, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilisema jana Jumanne.
Baadhi ya asasi za kiraia wilayani Kalehe inawalaumu vijana yenye silaha wanaojiita Wazalendo, ambao huzozana kila mara hadi kufikia kufyatuliana risasi katika baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo.
Soma pia:
Jumapili mchana, makundi manne yenye silaha yalipambana katika kijiji cha Bunyakiri ambako Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, Monusco, kilijiondoa wiki tatu zilizopita. Mapambano hayo yalisababisha kifo cha mpiganaji mmoja.
Asasi za kiraia zinaelezea kutokea matukio mengi kama hayo na zinayahusisha na kuripuka mara kwa mara kwa mabomu katika mipaka kati ya Wilaya ya Kalehe/Kivu Kusini na Wilaya ya Masisi/Kivu Kaskazini, hasa maeneo ya Ufamandu na Mupfunyi-shanga.
Eneo kulikotokea mapambano hayo yote ni mbali na kijiji ambacho watu saba waliuawa kwa mabomu.
Delphin Birimbi ni Msimamizi wa Mfumo wa mashauriano ya asasi za kiraia ndani ya wilaya ya Kalehe, anaiomba Serikali ichukue majukumu yake ya kuilinda ardhi ya Kongo kwa mujibu wa katiba ya nchi na kutafuta suluhisho la kudumu kwa suala la makundi yenye silaha yanayojiita Wazalendo kwa vile baadhi wanatatiza usalama wa raia:
Asasi za kiraia wilayani Kalehe zinaonya pia juu ya hali ya kibinaadamu inayozidi kuwa ngumu kwa wakimbizi waliotoka eneo la Masisi waliokimbia mapigano kati ya M23 na jeshi la Kongo, FARDC, na ambao bado wanakabiliwa na miripuko ya mabomu katika eneo walilokimbilia.