Wanaume wa ZNZ waruhusuni wanawake wang’ae kwenye tuzo

Mhandisi Zena Said ambae ni katibu kiongozi serikali ya Zanzibar amewataka wanaume wa Zanzibar kuwapatia fursa wake zao ili waonyeshe makubwa wanayoyafanya kupitia majukwaa, Katibu Kiongozi ameyasema hayo maara baada ya kupata taarifa baadhi ya wanawake walionyimwa fursa ya kuonesha makubwa wanayofanya kupitia malkia wa nguvu

Zena ameyasema hayo alipohudhuria kwenye Tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 ambazo kwa maara ya kwanza zimefanyika mbweni Zanzibar na Jumla ya Wanawake tisa wametunukiwa Tuzo ya Malkia wa Nguvu kwa makubwa wayafanyayo

kwa upande wake mwenyekiti wa Tuzo za Malkia wa nguvu Lilian Msuka amesema amejifunza mengi kati hayo ni kuona asilimia ya malkia wa nguvu wengi wa Zanzibar ni hupendi kuwashukuru waume zao kutokana na kuwepo mashirikiano ya kusaidiana

Nae Hijjab Dj maara baada ya Kunyakua Tuzo ya Malkia wa Nguvu 2024 amesema mtindo anaofanya wa kupiga mziki na kuvalia Hijabu ni kitu kipya licha ya Changamoto anazozipitia kwenye jamii ya Zanzibar kwa aina ya mtindo wa kazi zake

 

Related Posts