BRIGEDIA JENERALI MABENA AWEKA JIWE LA MSINGI MAHANGA YA VIJANA KIKOSI CHA 824 KJ KANEMBWA


Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Na.Alex Sonna-KAKONKO

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limeishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na majengo ili kuchukua vijana wengi wanaohudhuria mafunzo ya lazima kwa mujibu wa sheria pamoja na kundi la kujitolea

JKT ilikuwa na uwezo wa kuchukua vijana 5000 lakini kwa sasa inaweza kuchukua vijana 50,000 katika kundi hilo kwa wakati mmoja kutokana na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia kutoa fedha.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, wakati akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Brigedia Jenerali Mabena amesema Serikali imekuwa ikiendelea kufanya hivyo toka kurejeshwa kwa mafunzo ya kundi la kujitolea.

“Ikumbukwe wakati mafunzo yale ya lazima yanarejeshwa JKT ilikuwa na uwezo wa kuchukua vijana 5000 tu lakini kwa sasa inaweza kuchukua vijana 50,000 katika kundi hilo kwa wakati mmoja,”amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Amesema yote hayo yanatokana na JKT kuendelea kupewa fedha za maendeleo na Serikali.

Kuhusu kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Brigedia Jenerali Mabena,amesema wakati kikosi kinaanza kilikuwa hakina uwezo wa kuchukua vijana 1000 lakini kwa sasa kina chukua 4000 mpaka 5000.

“Na mimi niseme tu katika kikosi hichi tulichopo cha 824 Kanembwa Kakonko Mkoa wa Kigoma.Kikosi hichi tulikabidhiwa kutoka katika Kambi ya wakimbizi waliokuwa wanakaa hapa ilianza kuwa kiteule na baadae ikapewa hadhi ya kuwa kikosi,”amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Amesema kikosi hicho wameendelea kukiongezea uwezo kwa kuweka mahanga ya kulala vijana pamoja na bwalo na miundombinu mingine ambayo itatumika katika kulea vijana.

Brigedia Jenerali Mabena amesema katika mwaka wa fedha ambao utaishia Juni 30,2024 kikosi hicho kimepewa Sh bilioni 1.47 ambapo fedha hizo zinatumika kwa ajili ya kuhakikisha majengo yanakuwa sawa sawa.

Amesema katika fedha hizo kikosi kinaenda kutengeneza mahanga saba yenye uwezo wa kuchukua vijana 100 kila hanga moja.

“Kwa hiyo unaona tayari kutakuwa na ongezeko la vijana 700 katika ile idadi ya 4000 mpaka 5000,”amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Amesema kuna kituo cha Kiteule ambacho kipo Misenyi Mkoani Kagera kwa ajili ya shughuli za ufugaji

Amesema kule wana Kilimo,ufungaji pamoja na Uvuvi ambapo kitatumika kama sehemu ya kufugia na vijana watakitumia kupata mafunzo.

“Unaona kwa jinsi ambavyo Serikali imeendelea kutoa fedha na miundombinu inaendelea kukaa sawa na kuchukua vijana wote kwa wakati mmoja,”amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa fedha JKT,Luteni Kanali Eveline Kibisa amesema kama Mjumbe wa kamati ya fedha za maendeleo wanawapongeza wakuu wa vikosi sehemu zote walizopita kwani majengo yamejengwa vizuri na yanathamani.

Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa namna ambayo imewezesha kwani wameweza kuwapatia fedha za kutosha ambapo katika kila kikosi wameweza kuongeza idadi ya vijana.

“Nitoe rai kwa wakuu wa vikosi kuendelea kuzisimamia vizuri fedha hizo ili angalau Serikali ikiona kuna matumizi mazuri ipate moyo wa kuendelea kusapoti.”amesema Luteni Kanali Kibisa

Nay,Kamanda wa Kikosi cha 824 KJ, Luteni Kanali Mantage Nkombe,amesema katika kikosi hicho wamepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa mahanga saba.

“Tumeona ni mafanikio kwa sababu tunaenda kuongeza wigo na namba ya Vijana kujiunga JKT Kanembwa inaenda kuongezeka zaidi ya awali,”amesema Luteni Kanali Nkombe

Amesema kupitia fedha za maendeleo wanaenda kutekeleza miradi hiyo kwa kutekeleza maagizo kutoka Makao Makuu

“Kwa kuhakikisha majengo yanakamilika kwa wakati kulingana na fedha iliyotumwa na kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa na majengo yanajengwa katika ubora na kwa muda sahihi,”amesema

Amesema wanataraji ifikapo 30 June 2024 majengo yatakuwa yamekamilika kwa ajili ya vijana wapya ambao watakuja kujiunga na JKT katika kikosi hicho.

Kuhusu faida watakayopata katika miradi hiyo,amesema:”Kimsingi ni faida na kijana anapata ujuzi na ujuzi hauzeeki na ni manufaa kwake na atatumia kujiongezea kipato”.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akipokea taarifa ya ujenzi kabla ya kuweka wakati akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,(kulia) akipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.Kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha 824 KJ, Luteni Kanali Mantage Nkombe.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikagua maendeleo ya ujenzi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mkurugenzi wa fedha JKT,Luteni Kanali Eveline Kibisa,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi ujenzi wa Mahanga ya Vijana katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Related Posts