TASAC YANG’ARA TUZO ZA NBAA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeshika nafasi ya kwanza katika tuzo ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa mwaka 2023 kati ya Mamlaka 9 za Udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini.

Tuzo hiyo imepokelewa na CPA Pascal Kalomba Mkurugenzi wa Fedha kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum.

TASAC imeendelea kuchukua ushindi na kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo katika kipengele cha Mamlaka za udhibiti.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Muhasibu Mwandamizi Faustine Masalu amesema ushindi walioupata sio rahisi kwani wameshindana na taasisi nyingi lakini wamesalia katika ubora wao na kushinda nafasi ya kwanza.

Amesema ushindi huo unaonesha rasilimali walizopewa  na majukumu unaonesha jinsi ambavyo wanawajibika katika utekelezaji wa majukumu yao ambapo wamekuwa wakiyafanya kwa weledi 

Nae Mkurugenzi wa Fedha, CPA Pascal Kalomba ameongeza kuwa ili kuwa na maendeleo chanya katika usafirishaji wa majini taasisi yao inatakiwa kufuata misingi Bora ya kimahesabu ambapo hata taasisi za kimataifa zinapotazama





Related Posts