Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Rais Mstaatu Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Duru ya Nne na ya mwisho ya Mahafali ya 54 ya chuo hicho na kutunuku Shahada na Astashahada kwa wahitimu 2,069, ikiwa ni wanawake 1004 na wanaume 1065, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2024.Katika hizo ni shahada za Uzamivu 55, Shahada za Umahiri 449, Shahada za Uzamili 37, Shahada ya Awali 1,362, Shahada 116 na Astashahada. Picha na ISSA MICHUZI