Hamisa na Baba Levo washinda tuzo

Mwimbaji Star Clinton Levokatusi Chipando Maarufu Kama Baba Levo Pamoja na mrembo Hamisa Mobetto wameshinda tuzo ya Influencers Bora wa Mwaka kupitia tuzo za Consumer Choice Awards Africa zilizotolewa Usiku wa Jana

Baba Levo baada ya ushindi huo amefunguka kwa kusema “Mtanange ulikuwa Mzito sana, nawashukuru waandaaji wa Tuzo, ni mara yangu ya kwanza kugombea Tuzo, Sijawahi kugombea tuzo yoyote ile iwe Muziki au Uchawa, nimeingia na Kuchukua moja kwa moja, Namshukuru Diamond, Nashukuru makampuni yaliyoniamini kufanya nayo kazi, mimi Ndio influencer bora Tanzania nzima”

Na kwa upande wa Hamisa amesema kuwa “Miaka mitatu nyuma nilishinda tuzo ambayo nimekuja kushinda tena Usiku wajana, nawapongeza ma Meneja wangu ninao wawili, kwa mashabiki wangu Asanteni sana na kampuni ambazo mnaendelea kuniamini Asante sana”

Related Posts