AZAM FC imefikia makubaliano na Akademi ya Yeleen Olympique ya Mali kwa ajili ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Yoro Mamadou Diaby.
Mlinzi huyo wa kati ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye Klabu ya Stade Malien de Bamako, atajiunga rasmi na Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2024/25.
Akiwa Stade Malien de Bamako, Yoro aliisadia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, akiifungia timu yake mabao katika mechi zote mbili za robo fainali dhidi ya Dreams FC ya Ghana.
Yoro amezichezea timu zote za vijana za taifa za Mali, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23.
Pia alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Mali kilichoshiriki CHAN, mwaka 2022 nchini Algeria