Katika kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu, wadau mbalimbali wa elimu wamepongezwa kwa kuonesha juhudi juu ya kuhakikisha wafanikiwa kwa kuongeza miradi yenye kukuza sekta ya elimu.
Hayo yamebainishwa leo na Diwani wa kata ya Tangini, Mfaume Kamuga wakati wa mahafali ya Wanafunzi wa kabla ya shule ya awali pamoja na ufunguzi wa shule mpya ya Bright Aquity iliyojengwa Kibaha Picha ya Ndege katika Halmashauri ya Mji Kibaha ambapo amepongeza uwekezaji uliofanyika katika Halmashauri ya Kibaha Mji kwani itasaidia kukuza sekta ya elimu na hata Serikali pia imeweka mazingira kwa wadau na itaendelea kuboresha mazingira kwa wadau kukuza sekta ya elimu.
” Jambo hili kwetu sisi Viongozi wa Halmashauri ya Mji Kibaha tunasema ni maendeleo kujengwa kwa shule kwenye moja ya kata zetu ni njia ya maendeleo kwani itasaidia kuongeza ubora na ushindi katika sekta ya elimu ndani ya Halmashauri na hata mkoa wa pwani kwa jumla” Amesema Mfaume Kamuga.
Naye mkurugenzi wa shule ya Bright Aquity Saimon Msiyangi, amesema shule hiyo imejengwa kwa ajili ya kuendelea kuhudumia umma na kuendelea kuongeza nguvu katika sekta ya elimu kwani tayari tumeona mazingira ya uwekezaji yameboreshwa kwa kiasi kikubwa na yenye kusaidia kuongeza ubora na ubunifu katika elimu.
” Tumeanza na madarasa 6 lakini tunatarajia kuongeza kadri wanafunzi watakapoongezeka, lengo kubwa ni kuhudumia umma kama wanavyopenda huduma zetu za kule mbuyuni, ndio maana tukaamua tuwasogezee watu wa Kibaha “Amesema Saimon.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Bright Aquity ameishukuru serikali kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji katika Halmashauri ya mji Kibaha na kuiomba kuendelea kuboresha miundombinu kama maji, umeme hata Barabara ambavyo vyote katika mazingira ya elimu.