TCAA YATOA ELIMU SHULE YA SEKONDARI YA KIBASILA

 

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa elimu kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamkala hiyo kwa wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Kibasila na kuwataka kusoma masomo ya sayansi ili waweze kusomea masuala ya anga kwa lengo la kupunguza uhaba wa watalaam wa Sekta hiyo nchini. 

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo Afisa Mkuu Udhibiti Uchumi na Biashara kutoka Kitengo cha Uchumi  cha TCAA Eufrasia Bille amesema katika kuelekea kwenye maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Usafiri wa Anga  inayofanyika kila Desema saba kila mwaka wamekuja shuleni hapo ili kutoa elimu kuhusu Usafiri wa Naga ili kuleta uelewa kwa wanafunzi hasa wanaosoma masomo ya sayansi

Amesema  pamoja na mafanikio yaliyopo katika Sekta ya Anga ikiwemo kukuza uchumo lakini kama nchi imekuwa na uhaba wa watalaam wakiwemo marubani na mainjinia katika usariri wa anga hivyo Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wanafunzi kusoma taaluma hizo hasa wanawake.

“Katika nafasi yetu yakusherekea wiki ya Usafiri wa Anga duniani ambayo inafanyika kila mwaka  Desemba saba tunawaomba wanafunzi msome masomo ya sayansi ili muweze kuongeza idadi ya watalaam wa sekta ya anga nchini ambao wapo wachache hali inayosababisha Taifa kuingia gharama kwakuleta watalaam kutoka nje.

Amesema serikali kupitia TCAA imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuongeza watalaam ikiwemo kutoa ufadhili wa masomo katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kilichopo chini ya Mamlaka hiyo pamoja na nje ya nchi

Naye  Afisa  Mwandamizi Elimu na Uchechemuzi kutoka Baraza  la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC) Debora  Mligo amesema ili kuhamamisha wanafunzi kusoma masomo hayo walianzisha vikundi vya kitaaluma mashuleni ambapo pia vinaelemishwa kuhusu haki za mamlaka ya usafiri wa angana fursa mbalimbali zilizopo katika usafiri wa anga.

Afisa Mkuu udhibiti uchumi na Biashara kutoka Kitengo cha Uchumi TCAA Eufrasia Bille akitoa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha tatu wanaosoma masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari Kibasila ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Usafiri wa Anga duniani.

Afisa Mwanamizi Elimu na Uchemuzi kutoka TCAA- CCC  Debora Mligo akitoa elimu kuhusu namna abiria anavyoweza kupata msaada pale anapopata changamoto anapotumia usafiri wa anga hapa nchini kwa wanafunzi wa kidato cha tatu wanaosoma masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari Kibasila ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Usafiri wa Anga duniani.

Related Posts