Na Jane Edward, Arusha
Kongamano la 42 la kisayansi la chama cha kitaaluma madaktari wa wanyama Tanzania, linatarajiwa kufungulia na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan litakalohusisha Washiriki elfu mbili kutoka katika sekta za Wanyamapori na Mifugo kutoka nchi za Jumuiya ya Madola Mkoani Arusha.
Aidha Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Madaktari wa Wanyama nchini Tanzania (TVA) kwa lengo la kujadili kwa pamoja changamoto na kuona namna bora kuboresha sekta hiyo.
Profesa Esron Karimuribo ni mwenyekiti wa Chama hicho ambapo amesema Kongamano hilo la kisayansi litakalofunguliwa na Rais Samia lina umuhimu mkubwa kwa nchi na wananchi kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya Wanyama .
Ameongeza kuwa kongamano hilo litaangazia maeneo muhimu ya kuishauri Serikali jinsi ya kuboresha Sekta ya Mifugo nchini ili kufanya biashara nzuri ya mifugo Kitaifa na Kimataifa ili kukuza Uchumi wa Kaya na kuongeza Pato la Taifa kwa ujumla.
Awali kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa chama hicho Katibu wa Chama hicho Dk. Caroline Ulomi Uronu amesema Chama hicho kilianzishwa mwaka 1982 na kila mwaka kimekuwa kikifanya Kongamano la Kisayansi na mwaka huu litakuwa Kongamano la 42 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.