Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv
Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Yusuph Mwenda amesema wataendelea kutumia uzoefu wa wastaafu wa Mamlaka hiyo ilikuendelea kujiimarisha zaidi.
Alisema hayo jana Desemba Mosi, 2024 alipokuwa akizungumza katika siku maalumu ya Wana Jumuiya ya Wastaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Walipokutana kwa ajili ya kufurahi pamoja na kubadilishana mawazo.
Amesema kuwa kazi ambayo wastaafu hao waliifanya ni kubwa….”Tunawathamini sana Taasisi inaendelea kufanya vizuri kama mlivyokuwepo ila tuna vijana wengi wadogo wadogo ambao labda kwa kushindwa kuwatumia nyie mje kuwa kanseli wanashindwa kubadirika kuwa kama ambavyo mlikuwa nyie” amesema Mwenda
Amesema pamoja na mambo mengine wastaafu wanaweza kuisaidia TRA katika shughuli mbalimbali ikiwemo kuwanoa wafanyakazi vijana kwenye maadili pamoja na kuwashauri masuala mbalimbali ili nao waje wastaafu kwa heshima , Amani na Afya nzuri.
Mwenda amesema wastaafu hao wanaweza kuchangia mawazo yao kwenye Tume aliyoiunda Rais kwa ajili ya kupitia mifumo ya kikodi nchini.
” Mnaweza kutusaidi mmesikia Rais ameunda tume kwa ajili ya kupitia mifumo ya kikodi mimi naamini watu ambao wanaweza kuisaidia ile tume ni nyie wastaafu”
Amewaomba wastaafu hao kuendelea kuwa mabalozi na wahamasishaji katika suala la ulipaji wa kodi kwa malengo ya kuinua uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Kamishna Mstaafu wa taasisi hiyo,Harry Kitilya amesema amefurahi kukutana na wafanyakazi wenzake waliofanyakazi pamoja na kuacha alama kwenye jamii.
“Mmefanya kazi kubwa iliyotupa heshima mimi mpaka sasa nikipita barabarani wananiita bwana TRA,niwapongeze wafanyakazi wa TRA mliokuwepo kazini kwa kuendeleza uadilifu na usanifu,”amesema.
Kitilya amewataka waastafu kuaendeleea kuwa mabalozi wa Mamlaka hiyo pamoja na kuhamasisha watu walipe kodi na si kukwepa Kodi.
Naye Mwenyekiti wa Wastaafu hao, Julius Caeser amesema kuwa wamekutana ili kufurahi na kuweka kando msongo wa mawazo.
” Kama mnavyofahamu hili kundi limeunganishwa na mtandao … shughuli za mtandao hazitoshi tukaamua siku moja kwa mwaka tukutane…wengi wetu hapa wameshiriki kuanzishwa kwa mamlaka ya mapato,tuko tayari kutumika endapo TRA itakuwa ina jambo la uzoefu bado akili zetu ziko imara,” amesema Caeser.
Katibu wa Wastaafu,Yeremiah Mbaghi amesema wastaafu wanajivunia matunda waliyoyacha TRA na kwamba sasa kasi ya ukusanyaji kodi imeongezeka .
Aidha,ameshukuru hatua ya TRA kuimarisha dawati la kipekee kwa walipa kodi wakubwa ambalo lilikuwepo hapo awali lakini sasa limekuwa lakipekee.
Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya Wana Jumuiya ya Wastaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao walikutana kwa ajili ya kufurahi pamoja kuonana na kubadirishana mawazo. Hafla hiyo imefanyika Desemba Mosi, 2024. Jijini Dar es Salaam
Kamishana Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya akizungumza wakati wa hafla ya Wana Jumuiya ya Wastaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao walikutana kwa ajili ya kufurahi pamoja kuonana na kubadirishana mawazo. Hafla hiyo imefanyika Desemba Mosi, 2024. Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa wana Jumuiya ya wastaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Julius Caeser akizungumza wakati wa hafla ya Wana Jumuiya ya Wastaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao walikutana kwa ajili ya kufurahi pamoja kuonana na kubadirishana mawazo. Hafla hiyo imefanyika Desemba Mosi, 2024. Jijini Dar es Salaam
Katibu wa wana Jumuiya ya wastaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yeremiah Mbanghi akizungumza wakati wa hafla ya Wana Jumuiya ya Wastaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao walikutana kwa ajili ya kufurahi pamoja kuonana na kubadirishana mawazo. Hafla hiyo imefanyika Desemba Mosi, 2024. Jijini Dar es Salaam