Na. Vero Ignatius Arusha.
Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Umoja wa jumuiya ya Wahasibu wa Nchi za Afrika (AAAG)Umefanyika Jijini Arusha katika kituo cha kimataifa AICC ukiwa unaakisi matarajio ya pamoja kama mataifa ya Afrika ya kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha kama chachu ya ukuaji endelevu.
Akuzungumza wakati wa kuzungumza leo 2 desemba ,2024 wakati akifungua mkutano huo Waziri wa Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa aliyemuwakilisha Waziri mkuu ameitaka Jumuiya hiyo kuona namna ya kukuza ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, Sekta Binafsi na Asasi za kiraia, katika usimamizi wa fedha za umma hasa katika kutekeleza miradi ya maendeleo endelevu ili isaidie ufanisi na uthabiti katika utekelezaji wa miradi.
Bashungwa amesema kuwa Jumuiya inalenga kukuza na kuimarisha mifumo bora,ya usimamizi wa fedha za umma katika nchi z za Afrika ili kuhakikisha kwamba,fedha za umma zinatumika kwa njia inayozingatia uwazi, ufanisi, na uwajibikajiuwajibikaji
“kwa upande mwingine, Wahasibu Wakuu wa Serikali mna jukumu la kuongoza mageuzi katika mifumo ya kifedha ambayo itachochea ukuaji endelevu, kupunguza umaskini, na kuhakikisha kwamba rasilimali zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi”
Aidha amesisitiza ili kujenga imani ya umma, mifumo ya kifedha inapaswa kuwa ya kisasa, na inayokabiliana na
changamoto mpya Afrika inashuhudia maendeleo ya kiteknolojia, na ongezeko la mahitaji ya huduma bora za umma.
Ma kusema muhimu sana kujikita katika teknolojia na ubunifu ili kuboresha mifumo yetu ya usimamizi wa fedha, kuhakikisha
uwazi na uwajibikaji kwa umma.
Sambamba na hayo Bashungwa aligusia masuala ya mabadiliko ya tabianchi,na kusema kuwa kupotea kwa bioanuai, na uharibifu wa mazingira vinaonyesha uhusiano mkubwa kati ya mifumo ya kiuchumi, kijamii, na kimazingira.
“Hivyo, ni jukumu letu kuhakikisha maendeleo endelevu yanafikiwa kwa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, na asasi za kiraia, kwa kufanya uwekezaji rafiki kwenye mazingira,na kuwa na uhasibu endelevu ili kulinda uchumi na mazingira,Teknolojia za kijani na nishati jadidifu, ni chachu kwa maendeleo endelevu barani Afrika, na tunapaswa kuzitambua katika mifumo yetu ya fedha”alisema.
Kwa upande wake waziri wa fedha Dkt Lameck Mchemba amesema , zile 4R za Mhe. Dkt. Samia Suluhu ambaye amejizatiti kuliongoza taifa na kuhakikisha ustawi wake kupitia mkakati (Reconciliation, Reforms, Resilience and Rebuilding). Makakati huo ni mwongozo thabiti unaomsaidia kuunganisha jamii, kuimarisha taasisi, na kuweka msingi madhubuti kwa mustakabali wa taifa .
“Makakati huu wa 4R, ni mwongozo thabiti unaomsaidia kuunganisha jamii, kuimarisha taasisi, na kuweka msingi madhubuti kwa Mustakabadhi wa Taifa Kupitia Maridhiano ya Mheshimiwa Rais anaendeleza umoja kwa kuziba tofauti na kuleta mshikamano wa kitaifa”
Amesema Kupitia Maridhiano, Mheshimiwa Rais anaendeleza umoja kwa kuziba tofauti na kuleta mshikamano wa kitaifa. Kujitolea kwake kwa Mabadiliko kumeleta mageuzi muhimu ndani ya taasisi zetu, na kuongeza uwazi, uwajibikaji, na ufanisi katika usimamizi wa fedha za umma
Aidha Mkutano umehudhuriwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika ambapo umelenga kuwakutanisha Wahasibu Wakuu wa Serikali na wadau ili kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa fedha za Umma barani Afrika.
Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo “Kujenga Imani ya Umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu.” Kaulimbiu hii ni nguzo muhimu katika kukuza uwazi, uwajibikaji, na umakini katika matumizi ya fedha barani Afrika. Vile vile, inaakisi matarajio yetu ya pamoja kama mataifa ya Afrika ya kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha kama chachu ya ukuaji endelevu.