Na Said Mwishehe,Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete,amesema Serikali imepanga katika awamu ya kwanza kurasimisha watu milioni 13 kwa kuwaweka katika sekta rasmi wakati lengo la
mpango huo ni kurasimisha watu milioni 35.
Waziri Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa utafiti wa Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa uliofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mkoani Kigoma uliohusisha na kuzungumza na Vijana wanaofanya shughuli za kiuchumi nje ya Mfumo usiorasmi amesema mradi huo utawezesha kuwaweka watu wote katika Mfumo rasmi na kuwezesha pande zote kunufaika.
Amesema kuwa hivi sasa kuna biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zinafanywa nje ya sekta isiyorasmi hivyo sasa Serikali imekuja na Mpango wa Kitaita wa Urasimishaji sekta isiyorasmi (NIS) kuwezesha kurasimisha shughuli hizo ambazo zinawaingizia watu kipato.
Waziri Kikwete amesema kuna biashara nyingi zinazohitaji kurasimishwa ili kuchangia maendeleo na ustawi wa nchi bila hatua hiyo.”Tunahatarisha kuwa na watu binafsi wanaoendesha biashara lakini hawachangii taifa huku tukishutumu serikali kwa kupuuza.”
Amesisitiza kupitia mpango wa NIS watu milioni 35 watakuwa katika sekta rasmi na kwa kuanza watasajili watu milioni 13 .Ni mpango mkubwa utakapofanikiwa na kukamilika,utakuwa mpango mkubwa na namba moja kwa Afrika kwa kuwezesha watu milioni 35 kuwa katika sekta rasmi. “Wananchi watanufaika na Serikali nayo itanufaika.”
Akifafanua zaidi Waziri Kikwete amesema wanaofanya hizo biashara zisizo rasmi waweze kuwa sehemu ya wanaofurahia matunda ya nchi yao kwasababu leo hii kuuza mboga mboga, kufanya Shoe Shine , kuuza pipi na kuuza matunda sio laana bali ni sehemu ya kutafuta lakini mwisho wa siku kwa nchi yoyote inayoendelea ni lazıma biashara hızo ziwe na mchango fulani katika nchi , hata ikiwa ndogo lakini ichangie kitu fulani.
“Kwahiyo Serikalli ilipokuja na Mfumo huu wa NIS malengo yake makubwa inataka tuone hawa watu ambao wanaishi katika hii sekta isiyorasmi kwa namna moja au nyingine wanaweza kutusaidia kuwa na mchango katika nchi lakini nchi kwa upande wa pili nayo ithamıni mchango unaotolewa
“Ndio maana Serikali ilipokuja na mpango huu moja ya faida ambazo tunakwenda kuzipeleka katika eneo la biashara isiyorasmi tunalenga kuwapeleka katika mfumo uliorasmi, wawe na mchango chanya lakini Serikali nayo iwaangalie kuhakikisha wanapopata changamoto basi zinapatiwa ufumbuzi.
“Hapa tunapozungumza sasahivi Serikali kupitia NSSF tumekiwshaanza kuwaorodhesha na tunatarajia mpango huu utakapokuwa umekamilika katika picha kubwa tutakuwa tumesajili watu milioni 35 ,hivyo mnaweza kuona huu mpango unaweza kuwa mpango mkubwa kuliko mpango wowote uliowahi kufanyika katika Afrika ,kwa jinsi tulivyojipanga na tunavyotarajia utakuwa mpango mkubwa.”
Kuhusu utafiti huo,Waziri Kikwete amesema wanategemea tafiti Kama hao kuangalia namna ya kuendelea kutafuta utumbuzi wa changamoto za kundi hilo la watu ambao hawako katika sekta rasmi.”Lakini tunategemea tafiti kama hızı pia tuuangalie tunakwenda kuwakuta vijana wa namna gani na wako katika mazingira tuweze kuwapanga na kuwasajili ili nao wapate manufaa ya Taifa hili la Tanzania
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Kazi Duniani(ILO) nchini Caroline Mugalla, ameeleza Afrika inaongoza kwa nafasi kubwa zaidi ya ajira zisizo rasmi duniani, ambapo karibu asilimia 80 ya shughuli zinafanya kazi nje ya sekta rasmi.
Amesema kuwa changamoto hiyo inajitokeza hasa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo shinikizo la demografia linafanya uchumi usiokuwa ŕasmi kuwa mgumu kudhibiti. Wafanyakazi katika sekta hii mara nyingi wanakabiliwa na mishahara duni, ulinzi mdogo, na kuzuiwa kwa huduma muhimu,” alisema.
Wakati huo huo Suzanne Doran ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), alieleza kutokuwa rasmi kama sifa ya kubainisha uchumi wa Tanzania, kutoa riziki kwa mamilioni ya watu wasioweza kupata ajira rasmi.
Ameongeza wakati sekta isiyo rasmi ina jukumu muhimu katika kupunguza ukosefu wa ajira na kuunda ajira, wafanyakazi katika sehemu hii mara nyingi wanakabiliwa na uzalishaji mdogo na kukosa upatikanaji wa ulinzi wa kijamii na manufaa.
Akizungumza kuhusu utafiti uliofanywa Kigoma , Annamerick Aga ambaye ni Mtalaam wa Uchumi usiorasmi Shirika la Kazi Duniani amesema wwmefanya utafiti katika Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma kwa ajili za kuzungumza na Vijana wanaofanya kazi katika uchumi usiorasmi kuona changamoto zao na ni namna gani wanahitaji Serikali iwasaidie kwakuwa wanafahamu Serikali inampango wa kurasimisha biashara zote kwamba wao wanaoanaje
“Lakini Shirika la Kazi tuliona kabla ya kupeleka ujumbe wa kurasimisha biashara ni vema tukawaelewa wao wako wapi , wanafanya kazi katika
mazingira gani halafu ndio twende na ule ujumbe wetu wa kurasimisha.Hivyo tumekutana kwa ajili ya kushirikiana na wenzetu matokeo ya utafti na hapo tunakaona kuna changamoto ambazo vijana wanakabiliana nazo yakiwemo ya majukumu ya kuhudumia famia,kutakuwa na uwezo wa kukuza biashara.”
Alıpoulizwa kwanini wamechagua Mkoa wa Kigoma, amesema haikuchaguliwa tu na ILO bali mkoa huo umechaguliwa na Umoja wa Mataifa baada ya kufanyika utafiti katika mikoa yote ya Tanzania ni wapi wanaweza kuweka program zao.
Hivyo waliochagua Kigoma kutoka na mkoa huo kuwa nyuma kimaendeleo lakini ni mkoa unaopakana na nchi ya Congo ambayo sasa ni sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini kulikuwa na sababu nyingi lakini kwakuwa kigoma wengi wanasaidia waliona kwanini wasiungane kwa pamoja kusaidia huo mkoa.