Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema Wiki ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani ambayo inafanyika kwa mara ya nne yamepangwa kuanza Desemba 16 hadi 20 mwaka huu huku yakizinduliwa rasmi Desemba 17 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Desemba 2,2024 kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa Wilayani Kibaha, amesema maandalizi yamekamilika na yatafafanyika Viwanja Vya Mailimoja (Stendi ya zamani)
“Tumeandaa Wiki ya Viwanda Mkoa wa Pwani ambapo maonesho haya yatahusisha wenye viwanda wa ndanina nje ya Mkoa wa Pwani wanakaribishwa ili waweze kuonesha bidhaa zao wanazozizalisha”amesema Kunenge.
Mkuu wa Mkoa ameongeza kwa kusema kuwa maonesho hayo yatafunguliwa na mgeni rasmi ambaye atafahamika baadaye
Desemba 18, 2024 kutafanyika Kongamano maalumu lililopangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwamfipa Kibaha huku washiriki zaidi ya 550 wanatarajiwa kushiriki na kujifunza na kuona fursa mbalimbali zinazopatikana Mkoani hapa.
“Kwenye Kongamano hilo Viongozi mbalimbali kutoka serikalini, Mashirika ya Umma na sekta binafsi na wataalamu wabobevu ,wataalamu wa biashara na uchumi watakuwepo” amesema Kunenge.
Kunenge amesema kuwa Mkoa umejipanga vizuri kwa maonesho hayo ya Viwanda na biashara na wanatarajia
Viwanda 1,553 kushiriki huku Viwanda 78 vikubwa vimeanzishwa tangu Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani inakadiriwa watu 25,000 wanatarajiwa kuhudhuria maonesho hayo