SERIKALI nchini imesema kuwa itazidi kuimarisha matumizi ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu hususan kwenye eneo la Utafiti ili kutatua changamoto za kiuchumi na za kijamii nchini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yamesemwa leo tarehe 2 Desemba na Naibu Waziri Mkuu Dk. Dotto Biteko aliyemwakilisha Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kufungua kongamano na maonesho ya tisa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo ya matumizi ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuchangia kwenye uchumi shinda.
“Mimi nafarijika sana kuona kauli mbiu hii inakwenda sambamba na mpango wa maendeleo wa Taifa wa ulioanzia mwaka 2021 mpaka mwaka 2026 ”
Aliendelea “Pamoja na malengo ya mendelewa endelevu, hususan lengo namba nane, namba tisa, na namba 13 kuminatatu. Pamoja na ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020” alisema Dk. Biteko .
Amewahakikishia wanasayansi kuwa serikali inathamini mchango wao kwenye ujenzi wa taifa “niwahakikishie wanasayansi ,watafiti, wabunifu, na wadau wingine wote wa sayansi na teknolojia na ubunifu kuwa serikali yetu inawathamini sana mchango wenu kwa taifa kupitia tafiti na ubunifu wenu.
Matumaini yangu kuwa mtazidi kupanua wigo, watafiti, zinazojibu changamoto za kiuchumi, na za kijamii”, alisema Dk Biteko.
Dk Biteko amezitaja hatua ambazo serikali imezichukua katika kuimarisha mazingira mazuri kwa wanasayansi na watafiti kufanikisha malengo yao kwa lengo la kulisaidia taifa .
“Serikali kutoka mwaka 2021 mpaka sasa imetoa kiasi cha shilingi 32 Bilioni kupitia Costech kwa ajili ya utafiti katika sekta zaidi ya 20 ikiwemo , sekta ya Kilimo, uvuvi, elimu, ufugaji na Afya na Nishati.” Alisema Dk Biteko
Dk. Biteko amesema kuwa Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2022 serikali imevutia zaidi ya shilingi Bilioni 222.8 kutoka kwa wadau wa maendeleo .
“Sehemu kubwa ya matumizi ya fedha hizi zote ni katika kufanya tafiti kuboresha miundombinu ya utafiti na ubunifu , kuzalisha rasilimali watu na kujenga uwezo wa ubunifu wa kampuni changa ”
Amesema kuwa Serikali inatekeleza mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) wenye thamani ya shilingi Trilioni 1.13 .
“Fedha hizo kwa sehemu kubwa zinatumika kujenga na kukarabati na kuweka vifaa katika majengo 370 yanayojumuisha maabara na karakana 108 , kusomesha wahadhiri 526 kwenye ngazi ya umahiri na uzamivu na kuboresha mitaala takribani 563 ili kujibu mahitaji ya soko la ajira duniani pamoja na kuimarisha utendaji kazi wa COstech.
Amesema kuwa mashindano ya kitaifa ya sanyasi na Teknolojia na ubunifu yanayoendesha na Kituo cha Buni Hub iliyokuwa chini ya Costech ” kituo hiki kimesaidia kutengeneza kampuni ndogo zaidi ya 100 na kuwezesha ajira takribani 30,000 kongani bunifu 18 na kuchangia mapato ya taifa katika kodi ya wastani wa shilingi 500milioni”,amesema Dk. Biteko.
Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali imewatambua watafiti waliofanya tafiti zenye matokeo chanya.
“Tunataka watu wawatambue watafiti wetu waliofanya tafiti zilizoleta matokeo chanya hapa nchini ”
“Tunafanya hivi kama mwanzo wa kuzitambua tafiti za watafiti wetu.”
Wakati huo huo amemuomba Dk. Biteko kuzindua mfuko utakaowasaidia wabunifu kuingiza bidhaa zao sokoni.
Ametoa mfano wa mbunifu aliyetengeneza mita janja za maji iliyobuniwa na kijana wa kitanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) amesema kuwaimekuwa nchi yenye mafanikio kwenye utafiti hususan kwenye nchi za ukanda wa Sahara kutoka na kuwa na mifumo imara ya miongozo ya watafiti .
Dk. Nungu ambaye ndiye mwenyeji wa Kongamano hilo akiwakaribisha viongozi na washiriki kutoka nchi mbalimbali amesema kuwa Kongamano hilo lilihudhuriwa na zaidi ya taasisi 140 za nje na ndani ya nchi na litadumu kwa siku tatu na mada kuu ya Kongamano hilo ni ‘matumizi ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi’
Ameongeza kuwa COSTECH kupitia program mbalimbali imewasaidia vijana wengi kubadili ndoto zao kuwa fursa ambapo pamoja na mambo mengine imefikia uwezo wa kutoa vibali 1000 kwa watafiti kutoka nje ya nchi.
Balozi wa Norway nchini, Tine Tonnes ameipongeza Tanzania kufuatia hatua zake za kuendeleza watafiti na wabunifu huku akieleza utayari wa nchi hiyo kuendelea kuunga mkono program za uhifadhi wa mazingira.
Vikundi 19 vimepokea mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 6.3 ikiwa ni mkopo kwa watafiti, wabunifu waliofanya kazi inayosababisha matokeo..