Dar es Salaam. Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni na Ubungo, Boniface Jacob maarufu Boni Yai amekwaa kisiki baada ya Mahakama Kuu kumkatalia maombi yake kupinga amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, kulipa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni nywila (password) za simu zake.
Jacob, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani anakabiliwa na kesi ya jinai katika Mahakama ya Kisutu.
Katika kesi hiyo namba 26918/2024, anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.
Kufuatia kesi hiyo, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RCO), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) David Msangi aliwasilisha maombi akiiomba Mahakama imuamuru mshtakiwa kutoa nywila za simu zake mbili za mkononi kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma hizo.
Habari zaidi inakujia hivi punde