BOWMANS YASHIRIKIANA NA WADAU KUFIKISHA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA VIJIJINI TARIME

Wananchi wa kijiji cha Nyamwaga wakipata elimu ya utambuzi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ushauri wa kisheria

Wananchi wa kijiji cha Nyamwaga wakipata elimu ya utambuzi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ushauri wa kisheria

Wananchi wa kijiji cha Nyamwaga wakipata elimu ya utambuzi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ushauri wa kisheria

 

Baadhi ya mawakili wanaoendesha mafunzo hayo ( wa pili, watatu na wa nne) wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Maendeleo ya jamii (kulia) na baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Nyamwaga walioshiriki kwenye mafunzo hayo

 

Kampeni ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia, ukiwemo ukeketaji na ushauri wa kisheria inaendelea kufanyika katika kipindi hiki cha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo sasa inafanyika kijiji kwa kijiji ikiendeshwa na Kampuni ya masuala ya sheria ya BOWMANS ikishirikiana na Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

 

Wananchi kutoka vijiji mbalimbali wilayani Tarime wamekuwa wakihudhuria mafunzo yanayotolewa na wataalamu wa masuala ya madhara ya ukatili wa kijinsia na kueleweshwa masuala ya kisheria kutoka mawakili wa kampuni ya BOWMANS ambao wameenda wilayani Tarime kushiriki maadhimisho hayo.

 

Lengo la kampeni hiyo pia ni kuhakikisha kunakuwepo na dhana ya usawa katika jamii na haki inatolewa kwa watu wa tabaka la chini ambao hawana uwezo wa kulipa gharama za mawakili katika masuala mbalimbali ya kisheria.

 

Afisa Maendeleo ya Jamii, Msajili Msaidizi wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Mussa Maulid Magope, ametoa kwa wanavijiji kujitokeza kwa wingi kupata elimu na msaada wa kisheria kupitia kampeni hiyo.

 

“Natoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi ndani ya siku tano za kampeni hii katika vijijini 11 vinavyozunguka mgodi wa North Mara. Huduma hii ni bure, hakuna gharama yoyote,” alisema.

 

Kwa mujibu wa Magope, ni agizo na takwa la serikali la kuhakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zinapatikana maeneo yote nchini.

 

Wakazi wa vijiji ambavyo vimefikiwa na elimu hiyo wameeleza kuridhishwa na elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia, pamoja na huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa katika kampeni hiyo.

 

“Nimepokewa vizuri na nimepewa ufafanuzi zaidi. Nimefahamu kumbe hata sisi wanawake tuna haki ya kumiliki ardhi kama wanaume,” alisema Sara Joseph Magoko mkaza wa kijiji cha Nyamwanga.

 

Naye Patrick Ragita alisema: “Hii ni faraja kwetu wazee tusio na kipato cha kuwalipa mawakili kutusimamia kwenye kesi, tunaomba huu mpango uwe endelevu ili watu wa chini wasinyanyasike.”

 

Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ilizinduliwa Novemba 25, mwaka huu BOWMANS inashirikiana na VSO, Jadra, Life changing Foundation, Barrick, Taifa Gas na LCF.

Related Posts