Jesca kinara wa asisti BDL

WAKATI msimu wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) 2024, ukikaribia kumalizika, Jesca Lenga wa DB Troncatti   ndiye aliyekuwa kivutio kwa utoaji wa asisti tangu ligi hiyo ilivyoanza.

DB Troncatti ilitolewa na DB Lioness katika mchezo wa nusu fainali katika michezo 2-1 na mchezo wa kwanza DB Lioness ilishinda kwa pointi 64-45, mchezo wa pili Troncatti ikashinda 63-52 na wa tatu DB lioness ikashinda kwa 68-52.

Hadi DB Troncatti inatolewa nusu fainali, alikuwa anaongoza  kwa kutoa asisti mara 214, akifuatiwa na Tukusubira Mwalusamba wa Tausi Royals aliyetoa mara 137.

Jesca anayecheza namba moja ‘point guard’, anasifika kwa uwezo wake wa kumtoroka adui na kutoa pasi za mwisho, pia ana uwezo wa kumiliki mpira na nidhamu na ndiye aliyeongoza kwa kutokufanya faulo tangu ligi hiyo ianze.

Jesca pia alikuwa wa pili kwa kuiba mipira ‘steal’ akifanya hivyo mara 54 nyuma ya Tukusubira Mwalusamba wa Tausi Royals aliyepokonya mara 58.

Related Posts