Na Ashura Mohamed -Arusha
Afisa Mkuu wa Biashara kutoka Benki ya CRDB bw.Boma Rabala amesema Mkutano wa Pili wa mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu wakuu barani Afrika (AAAG) unaoendelea Jijini Arusha ni muhimu katika Sekta ya fedha ikiwa matumizi mazuri ya teknojia yatazingatiwa.
Ameyasema kayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Viwanja wa AICC ambapo amebainisha kuwa ikiwa kama wahasibu watahakikisha kuwa wanatumia teknolijia katika majukum yao hali ambayo itasaidia kuhakikisha wanadhibiti mianya ya upotevu wa mapato na si kutengeneza urasimu usio wa lazima.
Aidha amesema kuwa benki ya CRDB imefurahia kuweza kujumuika na wahasibu wakuu wa nchi za Afrika ambapo pia alipata fursa ya kuwasilisha Wasilisho lake na kuwashauri kuweza kuzishawishi nchi zao kuja kuwekeza nchini Tanzania.
“Ikumbukwe kuwa kila miradi inayokuwa inayotokea wahasibu wakuu wana majukum makubwa ya kutoa mipango na michango kwenye maamuzi mbali mbali yanayotokea pia wanaweza kuzishauri nchi zao kuja kuwekeza hapa nchini Tanzania,sasa sisi kama benki ya CRDB ambayo tuna mahusiano makubwa sana na Tanzania Investment Centre kwa ajili ya kuhakikisha tunawaleta wawekezaji nchini,tumeiona ni Vizuri kuwa wadhamini Wakuu wa Mkutano”alisema Rabala
Pia bw. Rabala alifafanua kuwa amepata nafasi ya kuwaelezea wateja ambao ni kutoka nchi mbali mbali barani Afrika namna ambavyo tunaweza kufaidika na kuwaleta nchini kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Moja ya sababu kubwa za benki hiyo kubwa hapa nchini kudhamini Mkutano huo mkubwa ni pamoja na kuendelea kutengeneza mahusiano mazuri kwa wateja wao na viongozi wanaotokea nje ya nchi, kwa kuwa Wahasibu wanasimama kwenye nafasi kubwa kwenye nchi zao ambapo kuna makampuni makubwa wanaweza kuyashauri kuja kuwekeza nchini Tanzania na Kupata huduma bora kutoka CRDB.