Mshindi wa shindano la Mama lishe msimu wa tano na mwanafunzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) Neema Mwang’onda amewaasa Wanawake wanaojishughulisha na biashara ya Mamalishe kutafuta ujuzi ili waweze kupika kwa viwango na ubora kukuza na kutangaza biashara zao
Amesema hayo Disemba 4, 2024 kata ya Mbagala wilayani Temeke jijini Dar es salaam, mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la Mama lishe lililohusisha upikaji wa kitafunwa maarufu Chapati na kujipatia kiasi cha shilingi laki 6 za kitanzania, kiwanja na baadhi ya vifaa vitakavyo muwezesha katika shughuli zake.
Mshindi huyo ameendelea kwa kuwatia moyo Wanawake hao waliojitokeza katika shindano hilo kutokata tamaa na waendelee kujitokeza kwani kupitia hivyo wanaitangaza pia biashara yao