Golikipa wa Simba, Hussein Abel amesafiri jana usiku kuelekea Algeria kuchukua nafasi ya Aishi Manula aliyekwama Dar es Salaam.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Manula kushindwa kusafiri na timu kutokana na kupata changamoto ya kiafya jana Jumatano Novemba 4, 2024 wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, muda mfupi kabla ya safari kuanza.
Manula alikuwa katika kikosi cha nyota 22 waliotakiwa kwenda Algeria ambapo Simba itacheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Costantine, Desemba 8, 2024
Katika eneo la kulinda lango, listi ya hivi sasa itakuwa na Moussa Camara, Ally Salim na Hussein Abel ambaye awali aliachwa.