EDWIN SOKO MWENYEKITI MPYA WA MISA – TAN

Mwenyekiti Mpya wa MISA- TAN Edwin Soko

Mwenyekiti Mpya wa MISA- TAN Edwin Soko

 

 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

 

 

Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) umefungua ukurasa mpya kwa taasisi hiyo baada ya Wajumbe kumchagua Edwin Soko kuwa Mwenyekiti wa MISA-TAN kwa kipindi cha miaka mitatu.

 

Edwin Soko anachukua nafasi hii kutoka kwa Salome Kitomari, ambaye ameiongoza MISA-TAN kwa mafanikio makubwa kwa kipindi cha miaka minane tangu mwaka 2018.

 

Uchaguzi huu uliofanyika leo, Jumatano, Desemba 4, 2024, katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma, unadhihirisha mabadiliko na uongozi mpya katika taasisi hiyo, huku Soko akitarajiwa kuendeleza na kukuza agenda ya uhuru wa vyombo vya habari na haki za wanahabari nchini Tanzania na katika kanda ya Kusini mwa Afrika.

 

Msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi, Ali Aboth, amemtangaza rasmi Edwin Soko kuwa Mshindi katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa MISA-TAN, baada ya kupata kura 33, akifuatiwa na Said Mmanga ambaye amekusanya kura 9, na Betty Masanja aliyepata kura 3 kati ya kura 46 zilizopigwa ambapo kura moja imeharibika.

 

Wajumbe wa Bodi waliotakiwa ni Wawili ambapo waliochaguliwa ni Alex  Benson Sichona  ambaye amepata kura 28 na Proper Kwigize aliyepata kura 31. Wengine waliokuwa wanagombea nafasi ya ujumbe ni Othman Maalim aliyepata kura 15, Isaack Wakuganda amepata kura nane na Juma Mudimi kura nane.

Mwenyekiti Mpya wa MISA- TAN ,Edwin Soko  (katikati) akiwa na wajumbe wa bodi waliochaguliwa , Alex Benson Sichona na Prosper Kwigize (kulia).

 

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Edwin Soko ameahidi kufanya mageuzi makubwa MISA – TAN ndani ya siku 100 kuanzia sasa.

 

Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa MISA – TAN, Salome Kitomari amewashauri viongozi wapya wa MISA – TAN kuendesha taasisi hiyo kwa kuzingatia Katiba na taratibu zilizopo.

 

Kama Mwenyekiti mpya, Soko anatarajiwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuimarisha demokrasia ya vyombo vya habari na kuhakikisha taasisi inakua na kuwa na ushawishi mkubwa zaidi katika masuala ya habari na mawasiliano katika kanda.

Msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi wa MISA – TAN , Ali Aboth akitangaza washindi uchaguzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya MISA – TAN

 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa MISA – TAN, Salome Kitomari akimpongeza Edwin Soko kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa MISA – TAN

 

Mwenyekiti Mpya wa MISA- TAN Edwin Soko akizungumza baada ya kutangazwa mshindi akiwa na wajumbe wa bodi waliochaguliwa , Alex Benson Sichona na Prosper Kwigize (kulia).

 

 

Mwenyekiti Mpya wa MISA- TAN Edwin Soko

Aliyekuwa Mwenyekiti wa MISA – TAN, Salome Kitomari akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 

 

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN  leo Jumatano, Novemba 4, 2024 katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma 

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 

 

Aliyekuwa mgombea uenyekiti MISA – TAN ,Said Mmanga

Aliyekuwa mgombea uenyekiti MISA – TAN Betty Masanja

 

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri na washiriki wa Mkutano wa MISA -TAN wakipiga picha ya pamoja

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri na washiriki wa Mkutano wa MISA -TAN wakipiga picha ya pamoja

 

Related Posts