Mkutano wa Mwaka wa Madini na Jiolojia wafanyika Tanga wasisitizwa kufanya utafiti na uvumbuzi wa rasilimali

Sekta ya madini nchini Tanzania kwa mwaka 2023/2024, makusanyo yameongezeka kwa asilimia 300 kufikia shilingi bilioni 700 kutoka bilioni 161 mwaka 2021. Ongezeko hili linaonyesha juhudi za serikali kupitia Wizara ya Madini katika kusimamia na kuendeleza sekta hii muhimu kwa uchumi wa taifa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhe. Msafiri Mbibo, amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa Jumuia ya wanajolojia unaofanyika siku sita Jijini Tanga ambapo amesisitiza umuhimu wa kutumia rasilimali madini kwa maendeleo endelevu na kulinda mazingira. Pia ameainisha kuwa mageuzi ya nishati kutoka matumizi chafu kwenda matumizi safi ni hatua muhimu, huku akitoa wito kwa wanasayansi kuendeleza utafiti na uvumbuzi wa rasilimali, kama vile gesi asilia.

Rais wa Tanzania Geologists Society (TGS), Dkt. Elisante Mshiu, alibainisha changamoto ya kutokuwepo kwa bodi ya usajili wa wanajiolojia, jambo ambalo linaweza kuathiri weledi na uaminifu katika tafsiri ya data na takwimu. “nahimiza kuanzishwa kwa chombo cha kusimamia weledi wa taaluma ya jiolojia ili kuhakikisha usimamizi bora wa rasilimali za madini”.

Kauli mbiu ya Mkutano wa Wanajolojia inasema kutumika utajiri wa Madini Kwa maendeleo ya kiuchumi ikiwemo kuhama kutoka nishati chafu na kwenda Matumizi ya nishati safi.

 

Related Posts