Mwalimu wa Neno la Mungu Emanuel Shemdoe akizungumza katika kuelekea mkesha wa mwisho wa mwaka utaofanyika Desemba Mjini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
MKESHA wa dini mbalimbli dini unatoa nafasi ya kuomba kwa ajili ya nchi na watu wote ikiwa ni pamoja na kumshukuru Mungu kwa Kuingia mwisho wa mwaka.
Mkesha huo utawapa watu kutafakari Matendo Makuu ya Mungu katika mwaka 2024
Akizungumza Katika Maombi ya siku 21 yanayoendelea hapo Dodoma, Mwalimu wa Neno La Mungu Emanuel Shemdoe,Amesema kua Mkesha huo utafanyika December 6 siku ya Ijumaa,katika Ukumbi wa Chuo cha Biblia cha TAG (CBC) Mipango jijini Dodoma ambao utaanza majira ya Saa 2 usiku
Amesema Katika Mkesha huo,Ni pamoja na kuliombea Taifa letu na Viongozi wake.
Neno Kuu la Mkesha huo ni Nimrudishie Nini Bwana ikiwa na Maana ya Kutafakari Namna ya Kumshukuru Mungu kwa Mwaka mzima.
Kwenye Mkesha huo,kutakua Na Waimbaji kutoka Chuo kikuu cha Udom(International choir social),Arusha Road kkkt Praise team,Cathedral Kkkt Praise team,na AIC choir Ipagala.
Hata hivyo,Mtumishi wa Mungub Dkt.Ipyana na Kundi la Essence of Worship chini MTUMISHI WA MUNGU Mtumishi Gwamaka Mwakalinga nao wataongoza sifa na ibada .
Pia mwimbaji wa mkongwe Upendo Nkone atakuwepo kuongoza ibada ya mkesha na mpigaji Sexaphone Moses Zamangwa.
Tunatarajia Kua na Viongozi wa Makanisa mbalimbali na Wa Serikali,katika kuungana kwenye ibada hiyo.