DKT.STERGOMENA AWATUNUKU WAHITIMU 9000 CHUO KIKUU UDOM

Na.Alex Sonna-DODOMA

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena  Tax,amewatunuku Wahitimu  9,000  wa chuo hicho katika Mahafali ya 15 mwaka huu.

Akitoa hotuba yake chuoni  hapo leo Disemba 5,2024 jijini Dodoma Makamu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka,amesema  kuwa takribani zaidi ya asilimia 80 ya wanaosoma katika chuo hicho wamefadhiliwa na serikali kupitia  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

“‘Hapa mmekuja kusoma mkimaliza mnaenda kuijenga nchi huo ndio utaratibu tulio nao, naomba niwahakikishie chuo hiki kinatoa elimu iliyobora  ndani ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na nyingine,” amesema Prof. Kusiluka.

Aidha amesema  utekelezaji wa miradi  chuo kimetekeleza miradi mbalimbali ikiwamo ya kiutafiti ambapo kwa sasa kina miradi 72.

Aidha,  Prof. Kusiluka ,amewataka Wahitimu hao wasichague kazi za kufanya kwa kuwa tayari wameshapata maarifa mbalimbali kupitia chuo hicho.

Awali Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Rwekaza Mukandala,amesema kuwa chuo kinaendelea kusimamia mikakati mbalimbali ya kiufanisi  na kwamba Baraza hilo linaendelea kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati wa chuo wa miradi iliyopo.

Prof. Mukandala ametoa shukrani zake za dhati kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeIea kukiunga mkono chuo hicho.

Aidha Prof Mukandala,amewapongeza Wahitimu wote kwa kumaliza masomo yao huku akiwataka kuwatumikia  wananchi na Taifa kwa ujumla.

Related Posts