Mtanzania atunukiwa udaktari wa heshima Uingereza

Dar es Salaam. Mtanzania Diana Laizer ametunukiwa udaktari wa heshima na Chuo cha Oxford Club Awards huko London nchini Uingereza kutokana na mchango wake kwenye jamii kupitia tuzo za Chaguo la Mtumiaji Afrika.

Diana ambaye ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa tuzo hizo maarufu Consumer Choice Awards, ametunukiwa udaktari wa heshima katika biashara na ujasiriamali kwa kuonesha jamii kuwa kijana anaweza kujitengenezea ajira na kuajiri wengine.

Akizungumza na Mwananchi, leo Alhamisi, Desemba 5, 2024 akiwa London amesema sababu nyingine ni pamoja na mchango wake kwa miaka sita kwenye tuzo hizo ambazo zimeongeza ushindani wa utoaji huduma bora kwa watumiaji hapa nchini na nje ya nchi.

Tuzo hizo zimelenga mtumiaji na mtoa huduma ili kuongeza thamani ya ubora wa bidhaa na huduma kati yao amesema: “Mchango wa ushiriki kwa miaka zaidi ya sita ndiyo chanzo kikubwa cha kupata udaktari wa heshima.”

Aidha kitendo cha kuthubutu kujiajiri, kutengeneza ajira kwa wengine na taasisi hiyo kuajiri vijana, kutambua mchango wa tuzo hizo kwa wafanyabiashara na uwekezaji hapa nchini ni miongoni mwa mambo yaliyombeba.

Amesema tuzo hizo zimekuwa mlango wa kufungua fursa kwa uwekezaji kwakufanya kazi na taasisi za Serikali na binafsi na hususani kutoa huduma kwa mtumiaji wa bidhaa hizo ikiwemo usafiri na afya.

Diana ambaye mzaliwa wa Arusha nchini Tanzania amesema tuzo hizo ziinamlenga mtumiaji na muuzaji kwa namna moja au nyingine na kuwa wanaendelea kutengeneza jukwaa la kuleta wageni kutoka nje ili kujishindia tuzo hizo.

Pia, kutambua mchango wa tuzo hizo katika uwekezaji kwa kufungua mlango wa uwekezaji nchini.

Related Posts