Ugonjwa wa uti wa mgongo nchini Niger waua watu 143,kampeni ya chanjo yaanzishwa

Wakati janga la sasa la uti wa mgongo nchini Niger limesababisha vifo vya zaidi ya watu 143, kampeni kubwa ya chanjo iliyozinduliwa Niamey, mji mkuu wa nchi hiyo, na Shirika la Afya Duniani (WHO) inatarajia kubadili mkondo wa maambukizi.

Mwandishi wa Africannews Joel Honore Kouam anaripoti kwamba watu wa Niger wanasubiri kwa subira kurejea kwa msimu wa mvua ambao wanaamini kuwa unaweza kusaidia kukomesha wimbi hilo kama ugonjwa wa meningitis – maambukizi ya utando mwembamba unaozunguka ubongo na uti wa mgongo  ni ya msimu.

Ugonjwa huu umeenea katika Sahel (eneo lenye ukame linaloenea kupitia Mali, Niger, Chad, na Sudan), hasa katika msimu wa kiangazi kuanzia Novemba hadi Mei ambao huja na vumbi, upepo, na usiku wa baridi.

“Inapaswa kusemwa kwamba mamia yao (Waniger) wanajitokeza katika kila kituo cha chanjo cha jamii ili kupokea dozi yao.

‘Kwa hivyo, wengi wanatarajia kampeni hiyo kuenezwa nchini kote katika siku zijazo” Kouam

Related Posts