CHAMA cha Wananchi CUF kinataraji kufanya mkutano Mkuu wake tarehe 18 na 19 Desemba mwaka huu huku ajenda kuu ikiwa ni uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike tarehe 13 Septemba uliahirishwa kwa kilen kilichosemwa kuwa upishaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa .
Wanacahama waandamizi wa chma hicho wamejitokeza kumkabili Mwenyekiti wa sasa Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alichukuliwa fomu ya kuwania tena nafasi hiyo.
Wanachama hao ni pamoja na mwanasiasa mkongwe Wilfred Lwakatare , Makamu Mwenyekiti-Bara wa sasa Maftaha Nachuma, Hamad Mohamed na Jafar Mneke.
Profesa Lipumba hajaweka hadharani kama ataendelea na kinyang’anyoro hicho au atatundika daruga.