Samatta aanza na asisti dakika 90 za kwanza PAOK

BAADA ya kupita mwezi mmoja na siku sita bila ya nyota wa kitanzania na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kucheza akiwa na PAOK ya Ugiriki, hatimaye mkali huyo alipewa dakika 90 uwanjani wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa 7-1 katika mechi ya hatua ya 16 Bora ya michuano ya Greek Cup Betsson.

PAOK ilipata ushindi huo dhidi ya Egaleo FC katika mechi hiyo iliyopigwa juzi, huku Samatta akitumika kwa mara ya kwanza kwa dakika zote 90 ikiwa ni zaidi ya mwezi mzima tangu alipoonekana uwanjani Oktoba mwaka huu.

Mara ya mwisho Samatta kucheza ndani ya klabu hiyo inayoshiriki ligi nchini Ugiriki ilikuwa Oktoba 30 akicheza kwa dakika 26 tangu hapo amekuwa akiambulia benchi.

Licha ya kuanza nyota huyo hakufunga bao katika ushindi wa mabao hayo lakini alitoa assisti ya bao mojawapo.

Chama hilo analolitumika Samatta, lipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 24 kwenye mechi 13 ikishinda saba, sare tatu na kupoteza michezo mitatu, huku rekodi zinaonyesha kuwa ndani ya mechi hizo nyota huyo amecheza dakika 116 zote dhidi ya PAE Egaleo ambazo timu hiyo imeshinda nyumbani na ugenini.

Kabla ya kuichezea PAOK nyota huyo wa zamani wa Mbagala Market, Simba na TP Mazembe ya DR Congo, aliwahi kupita kwa timu za Fenerbance ya Uturuki, Genk, Antwerp (Ubelgiji) na Aston Villa ya Uingereza.

Related Posts